AGOSTI 5, 2024
FILIPINO
Mafuriko Yatokea Sehemu Nyingi Baada ya Kimbunga Gaemi Kuikumba Filipino
Mwishoni mwa Julai 2024, Kimbunga Gaemi a kilitokea katika maeneo mengi magharibi mwa Bahari ya Pasifiki. Ingawa kimbunga hicho chenye nguvu hakikuipiga Filipino, kilitokeza mvua kubwa kuliko kawaida na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa, mafuriko, na maporomoko ya ardhi katika mji mkuu wa Manila na maeneo ya karibu. Inakadiriwa kwamba watu milioni 4.8 waliathiriwa. Zaidi ya watu 600,000 wamelazimika kuhama kutoka nyumbani kwao, na watu 39 hivi wamekufa.
Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata
Hakuna ndugu au dada aliyekufa au kujeruhiwa
Wahubiri 155 walilazimika kuhama kutoka nyumbani kwao, lakini wengi tayari wamerudi
Nyumba 2 ziliharibiwa kabisa
Nyumba 11 zilipata uharibifu mkubwa
Nyumba 42 zilipata uharibifu mdogo
Majumba 11 ya Ufalme yalipata uharibifu mdogo
Jitihada za Kutoa Msaada
Halmashauri 6 za Kutoa Msaada zimewekwa rasmi ili kuratibu kazi ya kutoa msaada
Waangalizi wa mzunguko na wazee wa maeneo hayo wanaandaa msaada wa kiroho na msaada wa kimwili kwa wale walioathiriwa na mafuriko
Tutaendelea kusali kwa ajili ya wote walioathiriwa na kimbunga hicho, na tutaendelea kumshukuru Yehova kwa kuwa ‘tegemeo imara la nyakati zetu’ kadiri anavyowategemeza na kuwatunza ndugu na dada zetu.—Isaya 33:6.
a Nchini Filipino kimbunga hicho kinajulikana kwa jina Kimbunga Carina.