Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Tabasamu

Tabasamu

Pakua:

  1. 1. Twaweza kusema mengi;

    Hadithi nyingi sana;

    Na tuchore picha nyingi,

    Je, watachochewa?

    Twaweza kusaidia

    Kwa neno na matendo,

    Ni tabasamu tu

    Tunalohitaji.

    (KORASI)

    Tabasamu itachangamsha.

    Tabasamu ni mwanzo muhimu.

    We usali utafanikiwa,

    Ya muhimu ni tabasamu tu.

  2. 2. Ulimwengu ni mwovu—na upendo hakuna.

    Wengi wametamaushwa dunia haijali.

    Tunaona nyuso zao wapitapo njiani.

    Hivyo tunawafariji tukikutana nao.

    (KORASI)

    Tabasamu itachangamsha.

    Tabasamu ni mwanzo muhimu.

    We usali utafanikiwa,

    Ya muhimu ni tabasamu tu.

  3. 3. Yasikitisha sana wanapokataa

    Wasiposikiliza ujumbe tuwapao.

    Na wengine ni wagumu kukubali ujumbe.

    Labda wanachohitaji ni tabasamu tu.

    (KORASI)

    Tabasamu itachangamsha.

    Tabasamu ni mwanzo muhimu.

    We usali utafanikiwa,

    Ya muhimu ni tabasamu tu.