JW LIBRARY SIGN LANGUAGE
Ongeza Nafasi Kwenye Kifaa Chako
Fuata hatua zifuatazo ili kuokoa nafasi kwenye kifaa chako na uweze kutumia vizuri kifaa kilicho na uwezo mdogo wa kuhifadhi.
Chagua ubora wa video
Kabla ya kupakua video, utachagua ubora wa video kwanza. Chagua video yenye namba ndogo zaidi katika orodha iliyoandaliwa ili usitumie nafasi nyingi katika kifaa chako. Ikiwa tayari ulikuwa umepakua video kwa kuchagua namba kubwa katika orodha iliyoandaliwa, unaweza kuifuta na kuipakua tena kwa kuchagua namba ndogo.
Dokezo: Kwenye skrini ndogo, kama vile ya simu, video yenye ubora wa 360p itaonekana vizuri. Lakini kwenye kompyuta au televisheni, ubora wa 720p ndio unaofaa zaidi.
Tazama video mtandaoni
Ikiwa una nafasi ndogo katika kifaa chako, jaribu kutazama video mtandaoni badala ya kuipakua. Ni lazima kifaa chako kiwe kimeunganishwa kwenye Intaneti ili ufanye hivyo.
Gusa popote kwenye video ili ianze kucheza.
Ikiwa utahitaji kutazama video hiyo wakati ambapo huna intaneti, gusa alama ya Pakua iliyo kama wingu. Ikiwa unatumia kurasa wa Biblia, chagua sura ili kuona orodha iliyoandaliwa ya ubora wa video.
Futa video zilizopakuliwa
Baada ya muda, huenda video ambazo hutumii kwa ukawaida zikawa bado katika kifaa chako. Fuata hatua hizi ili upate video hizo kisha uzifute:
Ingia sehemu ya Machapisho au sehemu ya Midia kisha bofya Zilizopakuliwa iliyo upande wa juu.
Bofya alama ya Mishale inayopishana. Katika orodha iliyoandaliwa, unaweza kuchagua neno Kubwa Zaidi ili video zinazochukua nafasi kubwa zaidi ziwe juu. Ukichagua neno Hazitumiwi kwa Ukawaida video ambazo hutumii sana zitakuwa juu kwenye ukurasa huo.
Ili kufuta video, bofya Nukta Tatu zilizo upande wa kulia wa video kisha ubofye Futa.
Pakua video na kuzihifadhi kwingine
Vifaa vingine vinaweza kukusaidia kuhifadhi video zako katika hifadhi ya kifaa hicho kwa kuhifadhi video hizo kwenye kadi ya ziada iliyoko kwenye kifaa (kadi ya SD) au mfumo wa ziada wa kifaa hicho.
Fungua sehemu ya Vipimo.
Bofya Hifadhi midia kwenye.
Chagua mahali ambapo ungependa kuzihifadhi.
Baada ya hapo video zote utakazopakua zitahifadhiwa mahali ulipochagua. Video zilizopakuliwa awali hazitahamishiwa mahali ulipochagua.
Vifaa vinavyotumia mfumo wa Windows, huenda havina chaguo la kuhifadhi kwenye kifaa hicho. Ikiwa hutapata mahali unapotaka kuhifadhi kwenye orodha iliyopo, fuata hatua zifuatazo:
Fungua folda na uteue tabo ya Mwonekano.
Bofya Kidirisha cha Uabiri na uhakikishe kwamba sehemu ya Onyesha Maktaba imetiwa alama.
Panua Maktaba kwenye orodha ya folda, bofya kitufe cha kulia kwenye kipanya chako juu ya folda ya Video kisha ubofye Sifa.
Ingiza habari kuhusu Mahali ambapo ungependa video unazopakua zihifadhiwe.